Matukio ya kisiasa

Matukio ya Afrika

Masuala ya jamii

Michezo

Habari kwa lugha ya Kiingereza

Tazama vidio 01:15
Sasa moja kwa moja
dakika (0)
Papo kwa Papo 19.09.2018 | 19.09.2018

Korea Kaskazini kuvifunga vituo vya kijeshi

Kinga imara mwilini kiboko ya Virusi na Bakteria

Mlo kamili wa kuvutia

Mfumo wa kinga unahitaji aina tofauti za mafuta. Unaweza kuyapata kutoka kwenye matunda na mboga. Mlo wako unapaswa kuwa wa afya na kuvutia: Machungwa, pilipili hoho, mboga za kijani na Kabeji nyekundu vinakupatia vitamini na pia vimesheheni vitamini C.

Kinga imara mwilini kiboko ya Virusi na Bakteria

Kimbiza virusi kila wakati

Tafiti za kisayansi zinapendekeza kwamba mazoezi ya mara kwa mara kama vile kukimbia, kutembea angalau mara tatu kwa wiki kwa dakika 20 kunaweza kuimarisha mfumo wako wa kinga. Lakini kuwa mwangalifu, usifanye mazoezi kupitiliza kwasababu pia unaweza kukausha mfumo wako wa kinga.

Kinga imara mwilini kiboko ya Virusi na Bakteria

Lala vizuri

Usingizi wa kutosha si tu unaruhusu mwili wako kurejesha nguvu. Wakati wa awamu ya usingizi ya mwendo wa polepole, neva zinaachilia na mfumo wa kinga unafanya kazi.

Kinga imara mwilini kiboko ya Virusi na Bakteria

Furahia maisha

Tafiti zinaonyesha kwamba ari nzuri na kufurahia maisha kunakuza mfumo imara wa kinga. Kucheka na kucheza si tu kunatoa mwanya wa maisha bora, pia kunaimarisha ulinzi wa mwili.

Kinga imara mwilini kiboko ya Virusi na Bakteria

Epuka msongo wa mawazo

Msongo wa mawazo unachochea homoni za adrenalin na cortisol. Homoni hizi zinaweza kupooza mfumo wa kinga. Kuepuka msongo na kuzingatia muda kunaruhusu mwili kupumzika na kuzalisha nguvu mpya. Mazoezi ya utulivu kama kutafakari, mafunzo ya tiba za kutuliza mwili na Yoga yanaweza kuimarisha mfumo wa kinga.

Kinga imara mwilini kiboko ya Virusi na Bakteria

Tembea!

Kutembea ili kupata hewa safi kunakupatia mabadiliko ya joto na mazoezi, vyote hivyo vinachochea mfumo wa ulinzi wa mwili. Tishu nazo pia hufaidika kutokana na mzunguko bora na unyevu unaongezeka hufanya iwe rahisi kupambana na mashambulizi.

Kinga imara mwilini kiboko ya Virusi na Bakteria

Chunga sana juu ya sukari!

Tafiti zinaonyesha kwamba kuunguza sukari ya muda mfupi kama fructose na glucose hutumia vitamini nyingi ambazo hazipatikani tena katika mwili.

Kinga imara mwilini kiboko ya Virusi na Bakteria

Maji ya moto na baridi!

Kubadilisha maji ya kuoga ya moto na baridi husaidia kudhibiti joto la mwili na kuboresha mtiririko wa damu. Kusugua mwili kutumia sponji pia huchochea mfumo wa kinga hata zaidi.

Albanian Shqip

Amharic አማርኛ

Arabic العربية

Bengali বাংলা

Bosnian B/H/S

Bulgarian Български

Chinese (Simplified) 简

Chinese (Traditional) 繁

Croatian Hrvatski

Dari دری

English English

French Français

German Deutsch

Greek Ελληνικά

Hausa Hausa

Hindi हिन्दी

Indonesian Indonesia

Kiswahili Kiswahili

Macedonian Македонски

Pashto پښتو

Persian فارسی

Polish Polski

Portuguese Português para África

Portuguese Português do Brasil

Romanian Română

Russian Русский

Serbian Српски/Srpski

Spanish Español

Turkish Türkçe

Ukrainian Українська

Urdu اردو